Karani mmoja wa kupokea wageni mjini
London alilazimika kurudi nyumbani baada ya kukataa kuvaa viatu vyenye
visigino virefu,imebainika.
Mfanyikazi huyo wa kampuni ya Temp,
Nicola Thorp mwenye umri wa miaka 27 kutoka Hackney aliwasili katika
kampuni moja inayoshughulikia maswala ya kifedha PwC kabla ya kuarifiwa
kwamba anahitajika kuvaa viatu vyenye visigino vya nchi 2 hadi 4.Alipokataa na kulalamika kwamba mbona wenzake wa kiume hawakutakiwa kuvaa hivyo,alitakiwa kurudi bila ya mshahara.
Kampuni ya Portico imesema kuwa iliweka sheria hizo kwa wafanyikazi wanaokabidhiwa PwC lakini imesema kuwa haitaondoa sheria hiyo.