Mamia ya ng'ombe na fahali walitembea kwenye jukwaa mwishoni mwa
juma katika mji uliopo kaskazini mwa India Rohtak katika maonyesho ya
aina yake ya urembo.
Hafla hiyo iliandaliwa na serikali ya eneo hilo kutoa mafunzo kuhusu aina tofauati za ng'ombe na haki za mifugo hao.
Zaidi ya ng'ombe 600 na fahali walishiriki na mmiliki ng'ombe aliyeshinda alijinyakuliwa zawadi ya dola 3,600.
Wakulima waliwasili na mifugo yao kutoka wilaya za jimbo la Haryana na
waliona fahari wakati ngo'mbe na fahali wao walipotembea juu ya jukwaa.
Huku wengine wakitembea bila matataizo na kwa madaha wengine walibidi kusukumwa ili wamalize.
Mafahali walikaguliwa kwa uzito, sura na ukubwa wa pembe zao. Na ng'ombe
walikaguliwa kutokana na uzuri wao na uwezo wao wa kutoa maziwa.
Waziri wa kilimo wa Haryana, OP Dhankar, alimtuza mmiliki ng'ombe aliyeshinda.
Wanafunzi
wa taasisi ya kimataifa ya elimu na utafiti wa mifugo sehemu ambako
maonyesho hayo yalifanyika, walipiga picha na ng'ombe walioshinda.
Anayedaiwa kumchoma moto mwanamke katika njia ya treni kufikishwa mahakamani
-
Mwanamume anayedaiwa kumchoma moto mwanamke aliyekuwa amelala hadi kufa
ndani ya treni ya chini ya ardhi ya Jiji la New York anatarajiwa kufikishwa
mahak...
16 hours ago