Recent Posts

PropellerAds

Monday, May 9, 2016

sheria mpya ziidhinihswe za kuyalazimu makampuni kutoa taarifa kwa umma

Kundi la wanauchumi 300 maarufu wameomba sheria mpya ziidhinihswe za kuyalazimu makampuni kutoa taarifa kwa umma za shughuli zozote za ulipaji kodi kutoka nchi moja hadi nchi nyengine.
Katika barua kwa viongozi wa dunia, kundi hilo limeomba Uingerez kuchukua uongozi wa hilo katika kushinikiza uwazi zaidi katika ulipaji kodi.
Nchi maskini ndio zinaathirika zaidi kutokana na ukwepaji kulipa kodi, wanadai.
Waandishi barua hiyo, iliyoratibiwa na shirika la misaada Uingereza Oxfam, wanajumuisha muandishi bora Thomas Piketty na mshindi wa tuzo ya Nobel ya Uchumi 2015 Nobel Angus Deaton.
Barua hiyo inajiri wakati mkutano wa seikali ya Uingereza wa kukabiliana na rushwa unatarajiwa Alhamisi, ambapo wanasiasa kutoka nchi 40 pamoja na benki ya dunia na shirika la fedha la kimataifa wanatarajiwa kuhudhuria.

"Tunahitaji makubaliano mapya ya dunia kuhsu masuala kama ya utangazaji wazi wa mataifa yakiwemo yanayotajwa kuwa ngome za ukwepaji kulipa kodi," wanauchumi hao wameandika kwenye barua hiyo.
"Ni lazima serikali ziwajibike kutakasa matiafa yao kuhakikisha maeneo yte wanayodhibiti wanatangaza kwa umma taarifa kuhusu wamiliki kampuni na wakfu," wameongezea.
Barua hii inajiri baada ya ufichuzi mkubwa wa nyaraka za siri za Panama zilizbainisha jinsi matajiri wanavyoficha mali, jambo lililozusha shutuma kali kwamba maafisa wa serikali wameshindwa kuchukua hatua.
'Athari kubwa'Oxfam linasema kwamba zaidi ya nusu ya makampuni yalioanzishwa na Mossack Fonseca, kampuni ya mawakili iliyo chanzo cha ufichuzi huo wa nyaraka za Panama, yameshirikishwa kuwepo katika maeneo ya ng'ambo Uingereza kama vile Virgin Islands.
"ili muradi ng'ome zinazotajwa za Uingereza zinaendelea kusaidia matajiri kukwepa kulip akodi itaendelea kuathiri pakubwa hadi ya Uingereza kama nchi kiongozi katika vita dhidi ya rushwa na umaskini duniani," amesema afisa mkuu mtendaji wa Oxfam, Mark Goldring.
Mwezi uliopita, mashrika ya kuidhinisha ulipaji kodi na sheria Uingereza, Ujerumani, Ufaransa Italia na Uhispania yalikubali kubadilishana data katika hatua mpya ya kuwasaka wakwepaji kulipa kodi kimataifa.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo mapya, mataifa hayo matano yatabadilishana taarifa kuhusu usajili wa wamiliki rasmi wa mali.