Recent Posts

PropellerAds

Wednesday, May 25, 2016

Watanzania 8 waliotaka kujiunga na al-Shabab wakamatwa

Serikali ya Kenya imefichua kwamba imewakamata
raia wanane wa Tanzania waliokuwa katika harakati za
kujiunga na kundi la wapiganaji la al-Shabab nchini
Somalia.
Katika taarifa iliotumwa katika vyombo vya habari,
polisi wanasema raia hao waliokamatwa katika kipindi
cha miezi miwili iliopita walikiri kuwa mbioni kujiunga
na kundi hilo la ugaidi.
Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya kundi la watu
wanaojidai kuwa wapiganaji wa Kiislamu kuweka video
mtandaoni likidai uwepo wa wapiganaji wa Kiislamu
nchini Tanzania
Video hiyo iliwaonyesha wanaume hao wakiwa
wamejifunika nyuso zao kwa vitambaa na barakoa.
Wanadai wamo katika mji wa Tanga na kuwahimiza
Waislamu katika taifa hilo la Afrika Mashariki kujiunga
na kampeni yao.
Wapiganaji wa Kiislamu wadai 'wamo Tanzania'
Polisi wa Kenya pia wanasema wamefanikiwa kutibua
njama ya wanachama wa kundi linalojiita Islamic State
ya kutekeleza mashambulio nchini humo na
kuwakamata washukiwa wawili.
Wawili hao Kiguzo Mwangolo Mgutu na Abubakar Jillo
Mohammed walipewa mafunzo ya kuwa na itikadi kali
kabla ya kuingizwa katika kundi la IS na Mohammed Ali
aliyekamatwa awali na ambaye anasaidia polisi na
uchunguzi, polisi wamesema.
Kulingana na taarifa hiyo, kufuatia kukamatwa kwa
Mohammed Ali, wafuasi wake wamekuwa wakipanga
kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi sana wakilenga
sekta ya uchukuzi wa abiria.
Kukamatwa kwa wawili hao, kumezuia kutokea kwa
mashambulio katika miji ya Nairobi na Mombasa.