Recent Posts

PropellerAds

Sunday, May 8, 2016

Magufuli aahidi sukari ya bei ya chini


Serikali ya Tanzania imeagiza sukari ilikukabiliana na upungufu wa sukari uliopo nchini.
Rais wa Tanzania Joseph Pombe Magufuli amesema badala ya kuwapa wafanyabiashara leseni ya kuagiza sukari kutoka ng'ambo serikali yenyewe ndio itaagiza sukari hiyo moja kwa moja.
Kauli hiyo inawadia baada ya mabohari zaidi kugunduliwa kote nchini yakiwa yamejaa sukari iliyoagizwa kutoka nje na ile iliyonunuliwa kwa wingi kutoka kwenye kampuni za kusaga sukari za humohumo Tanzania.
''Kuna mmoja ambaye amepatikana Arusha amehodhi zaidi ya tani elfu tano ya sukari naye mwengine huko Kilombero amenunua sukari yote kutoka kwa kampuni za humu humu nchini na akaficha.''
''Lakini hili ni swala la sasa tu, katika siku zijazo sukari itapatikana kwa wingi hapa Tanzania.Serikali imekwisha agiza sukari lakini hatutawapa hawa waliofilisi watanzania leseni ya kuingiza tena sukari.
''Serikali imeagiza na itauza sukari hiyo kwa bei ya chini,,,, hiyo ndio lengo la serikali '' alisema rais Magufuli huku mawananchi wakimshangilia.
Sukari hiyo ambayo huwa ni ya bei ya chini hubadilishwa na kisha kuvikwa magunia ya makampuni ya Kitanzania yanayosaga sukari na kisha kuuzwa rejareja.
Tumbua tumbua ya rais Magufuli imesadifiana na tangazo la Halmashauri ya ushuru ya Tanzania TRA kuwa imeanza kugawa sukari iliyoingizwa nchini kinyume cha sheria na kufichwa katika mabohari kote nchini.
TRA ilichukua hatua hiyo baada ya mwekezaji wa kibinafsi mkoani Lindi kupatikana na zaidi ya mifuko elfu tano za sukari kutoka nga'mbo.
Yamkini sukari hiyo hubadilishwa kwenye mifuko yenye nembo ya kampuni za kusaga sukari za Tanzania na kisha kuuzwa kwa bei maradufu

Related Posts:

  • How to Reset Your Joy in God You started last year with a tankful of gas — overflowing with energy, motivation, joy, and optimism. Twelve months on, you were empty, running on fumes, joyless, and dreading the new year. You wonder if you can even go an… Read More
  • I Can’t Do This, God Weak, low, despised and unlikely are essential qualities God looks for in his servants, and he chooses these qualities with great intentionality (1 Corinthians 1:27–29). Don’t believe me? Look at the odd list of qualificati… Read More
  • Ten Biblical Truths on the Obedience of Children Two years ago, I must have struck a nerve with the article “Parents, Require Obedience of Your Children.” It has proved to be one of our most visited resources. In view of that, I thought it might be helpful to go behind … Read More
  • God’s Favorite Prayer to Answer We took a knee. John Fogerty’s “Centerfield” or Alabama’s “Cheap Seats” would be playing over the loudspeakers. The crowd was settling into the bleachers. The infielders had finished up the final round of pregame grounders… Read More
  • Hear from God together. For the past ten years, I have done whatever I can to receive regular reproof from at least one other godly man. Because of what I have seen in the Bible, and because I have tasted the lasting fruit of real and consistent ac… Read More