Recent Posts

PropellerAds

Saturday, May 7, 2016

Urusi :Mkataba wa amani kuongezwa siku Aleppo

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema kuwa mkataba wa
usitishaji mapigano utaongezewa muda wa siku tatu
katika jiji la Aleppo na maeneo ya Kaskazini katika
mkoa wa Latakia.
Karibu raia 300 wamefariki chini ya muda wa majuma
mawili kutokana na makabiliano makali ya silaha.
Utulivu umetajwa kurejea katikati mwa Aleppo. Hata
hivyo makabiliano makali yangali yanaendelea Kusini
ambapo wanajeshi wa Syria na waasi wa Kiislamu
kukiwemo kundi la Nusra Front wamekuwa wakipigana.
Mapatano ya amani yalikuwa sehemu moja ya juhudi
za kujenga msingi wa kusitisha mapigano ulioanza
Februari mwaka huu.
Katika maeneo mengine ya Syria Kaskazini, kungali
kuna hali ya sintofahamu juu ya mashambulizi ya ndege
yaliyofanywa Alhamisi kwenye kambi za watu
waliotoroka makwao. Urusi na Serikali ya Syria
wamekanusha kuhusika.