Wanafunzi katika chuo kikuu cha
Dodoma nchini Tanzania wamefukuzwa chuoni humo baada ya kuzuka kwa
mgogoro kati ya serikali na wahadhiri wa chuo hicho.
Wanafunzi hao waliagizwa kuondoka katika chuo hicho kufikia saa kumi na mbili jioni siku ya Jumapili.Maelezo kuhusu mgogoro huo kati ya ya wahadhiri wa chuo hicho na serikali haujulikani.