Mazungumzo ya amani kuhusu Burundi yameanza mjini Arusha, Tanzania, baada ya kuahirishwa mara kadha.
Serikali
ya Burundi, na baadhi ya viongozi wa upinzani wanahudhuria mazungumzo
hayo, ambapo mpatanishi ni rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa.Lakini kundi kuu la upinzani halikujumuishwa, kwa sababu serikali imesema, haitozungumza na watu, inaowaona kuwa wapiganaji.
Mamia ya watu wameuwawa nchini Burundi, tangu Rais Pierre Nkurunziza kuamua kuania muhula wa tatu wa uongozi wa nchi.