
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali umesema kuwa walinda amani wake
watano wameuawa na wengine wamejeruhiwa vibaya katika shambulizi
lililotokea katikati ya mji wa Mopti. Waathirika wanatokea nchini
Togo.Gari lao lilipatwa na moto kabla ya kukanyaga bomu la ardhini,na
kisha kulipuka.Waziri wa masuala ya kigeni nchini Mali, Abdoulaye Diop,
ametuma salam za rambirambi katika mitandao ya kijamii kwa UN na nchi ya
Togo.Vifo vyao vimekuja wakati dunia ikiadhimisha siku yawalinda
amani.Mwaka uliopita walinda amani 129 kutoka umoja wa mataifa
walipoteza maisha katika nchi 16 wanazofanyia shughuli zao.