Recent Posts

PropellerAds

Saturday, May 7, 2016

SHEHENA KUBWA YA SUKARI ILIYOKUWA IMEFICHWA IMEFICHULIWA........

Taasisi ya kuzuia na Kupambana na rushwa
(TAKUKURU) imebaini kuwepo kwa sukari iliyofichwa
tani 4,579.2 iliyonunuliwa toka Kiwanda cha Sukari
Kilombero.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es
salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentine
Mlolowa Taasisi hiyo imeanza uchunguzi dhidi ya
swala hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa mnamo tarehe 05 Mei,
2016 timu ya uchunguzi ilitembelea maghala yaliyopo
Tabata Jijini Dar es salaam na kubaini uwepo wa sukari
hiyo.
TAKUKURU tayari imetembelea Maghala ya
mfanyabiasha Haruni Daudi Zacharia ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Al-Naeem yaliyoko Mbagala na
Tabata ambaye ni miongoni mwa wafanyabiashara
wakubwa wa sukari hapa nchini na anayetuhumiwa
kuficha bidhaa hiyo.
Aidha uchunguzi uliofanywa na Taasisi hiyo ulibaini
kuwepo kwa njama za dhati za kutouza sukari
iliyokutwa katika maghala hayo kulikofanywa na
mfanyabiashara huyo kwani hata sehemu ya Maghala
ilipo sukari hiyo hapakuwa na dalili za upakiaji wa
sukari hiyo ili iweze kusambazwa.
Taarifa hiyo imeendelea kufafanua kuwa katika eneo la
Kitumbini kumekuwa na wananchi wengi wanaohitaji
bidhaa hiyo na wachache sana waliweza kuuziwa licha
ya ukweli kwamba sukari ilikuwepo.
Katika uchunguzi wake TAKUKURU pia imebaini
kuwepo kwa mikakati ya dhati iliyokuwa ikifanywa na
mfanyabiasha huyo kwa kununua sukari yote toka
viwanda vya ndani na kisha kuihifadhi na kuuza bidhaa
hiyo kidogo kidogo kwa wastani wa tani 250 kwa siku
wakati alikuwa na uwezo wa kuuza zaidi jambo
lililochangia uhaba wa sukari katika soko.
Kuficha bidhaa ni kosa la uhujumu uchumi na ni
kinyume na Aya ya 3 Jedwali la kwanza Sheria ya
Uhujumu Uchumi Sura ya 200 [Chapisho la Mwaka
2002]. Serikali haitavumilia hujuma za namna hii na
itachukua hatua kali dhidi ya mfanyabiashara yeyote
ataekwenda kinyume na sheria hii.
TAKUKURU inatoa wito kwa wafanyabiashara wote wa
sukari kuacha vitendo vya kuficha sukari na vyombo
vya uchunguzi vinafuatilia kote nchini na yeyote
atakayebainika kufanya hujuma hizo atakabiliwa na
mkondo wa Sheria