Papa aliahidi kubuni tume kutafiti na kujadili uwezekano huo wa
kuwezesha wanawake kuhudumu katika ngazi hiyo ambayo ni daraja moja tu
chini ya makasisi. Wanahistoria wanasema zamani wanawake walihudumu kama
mashemasi.
Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, amesema ataunda tume
itakayochunguza na kujadili uwezekano wa wanawake kuteuliwa kuwa
mashemasi katika Kanisa hilo katika pendekezo linaloashiria uwazi wa
kuruhusu wanawake kuteuliwa kuhudumu katika nafasi ambazo zimekuwa za
wanaume pekee. Wazo hilo tayari limeanza kuibua hisia mbalimbali.
Ni katika mkutano wake maalum na waumini wanawake 900 waliojumuika
Vatican ambapo katika awamu ya maswali, suala hilo likaibuka. Papa
aliulizwa ikiwa atakuwa radhi kuruhusu utafiti kufanywa kuhusu uwezekano
wa wanawake kuwa mashemasi, jambo ambalo ni kinyume na kanuni za sheria
za kanisa hilo. Papa aliahidi kubuni tume kutafiti na kujadili
uwezekano huo wa kuwezesha wanawake kuhudumu katika ngazi hiyo ambayo ni
daraja moja tu chini ya makasisi. Wanahistoria wanasema zamani wanawake
walihudumu kama mashemasi.
Robert Gahl ambaye pia ni kasisi na pia profesa wa maadili katika chuo
kikuu cha kikatoliki Pontifical University of the Holy Cross anasema
"Kile ambacho Papa anatafakari ni uchunguzi wa kihistoria kuhusu
majukumu ambayo mashemasi wanawake walikuwa wakifanya, na kufikiria
kuyazingatia ili kuwezesha wanawake katika njia moja ya ushemasi. Hata
hivyo tutarajie kuwa papa hatahimiza kitu kama hicho kwa sababu tayari
ameshasema hataki wanawake kuwa makasisi. Analotaka ni kuwezesha
wanawake katika jamii".
Kauli ya Papa ilipokelewa vema na baraza la kutawaza wanawake WOC,
shirika la Marekani linalohimiza kanisa katoliki kuanza kutea na
kutawaza wanawake katika ngazi zote za huduma kanisani ikiwemo ukasisi.
Papa Francis ameonekana mara kwa mara akihimiza usawa wa kijinsia. Kate
Mc Elwee ambaye ni mkurugenzi wa baraza la uteuzi wa wanawake, ni kati
ya wale ambao wamesifia kauli ya Papa kwa kukubali mjadala huo ufanywe.
Amesema "Ninafikiria kuwa Papa kweli anataka swali hilo lijadiliwe.
Maandiko yetu wenyewe na wahubiri wametuambia kuwa wanawake sawa na
wanaume wamekuwa mashemasi tangu zamani, kwa hivyo ninafikiria tume
itaunga mkono historian a itakuwa bora ikiwa Vatican itakubaliana na
hilo"
Mashemasi hutawazwa kuwa wahudumu tu wa kanisa lakini si makasisi. Japo
wanaweza kutekeleza majukumu mengineyo yanayofanywa na makasisi, kama
vile kuongoza sherehe za harusi, ubatizo na hata kuhubiri, hawawezi
kuongoza misa ya Pasaka.
Kadhalika amerudia mara kwa mara kuwa hataki kuwakilisha mafunzo yote ya
kanisa kana kwamba yameandikwa kwenye jiwe. Amejaribu kufanya kanisa
kuwa na uelawa na kutofanya maamuzi dhidi ya waliotalikiana,
wanaowekeana kimada na waumini ambao ni wapenzi wa jinsia moja
Simba SC kwa kushirikiana na Mo Dewji Foundation wamerejesha kwa Jamii
kabla ya mchezo wao na Bravos
-
Kuelekea mchezo wa kwanza wa hatua ya Makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika
wa Simba SC dhidi ya Bravos ya Angola utakaochezwa Novemba 27, Simba SC kwa
k...
10 hours ago