Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Hamis Kigwangalla, amemtaka
mtangazaji wa Clouds FM, Gardner G Habash
kumuomba radhi aliyekuwa mke wake, Lady Jaydee
kwa ‘kile alichokiita’ kama udhalilishaji kwake na kwa
wanawake wote.
Wikiendi iliyoisha imesambaa video mtandaoni
ikimuonesha mtangazaji huyo akiongea kwenye
tamasha alilokuwa mshereheshaji: My name is Captain
Gardner G Habash all the way from Clouds FM, Jahazi
hatari sana. Na sina neno na yule mtoto wa kike.
Nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi.”
Video hiyo imesababisha hasira kubwa kwa mashabiki
wa Jaydee na watu wengi kwa ujumla.
“Ndg. Gardner amefanya udhalilishaji mkubwa si tu
Kwa @JideJaydee bali ametukana wanawake wote.
Mimi #BaloziWaWanawake namtaka aombe radhi,”
ameandika mheshimiwa Kigwangalla kwenye Twitter.
“Natoa rai kwa uongozi wa @cloudsfm kumtaka Ndg.
Gardner afute kauli yake na aombe radhi kwa
@JideJaydee na kwa umma ili kulinda heshima yao,”
ameongeza.
“Jamani, sijui ugomvi wao wala sina interest ya kujua,
sema alichokisema G na nikasikia ni katika
tusiyosemaga hadharani kwa heshima ya mama,”
amefafanua.
“Sina maana wamchukulie hatua. Watambue tu kosa
lake na wamtake kwa heshima kwa mama aombe
radhi. Mimi ni mtumishi namba 2 kwenye Wizara
inayosimamia ‘mambo ya wanawake’! I know what I
am talking about hapa.”
Anayedaiwa kumchoma moto mwanamke katika njia ya treni kufikishwa mahakamani
-
Mwanamume anayedaiwa kumchoma moto mwanamke aliyekuwa amelala hadi kufa
ndani ya treni ya chini ya ardhi ya Jiji la New York anatarajiwa kufikishwa
mahak...
15 hours ago