Ujumbe uliowekwa kwenye mtandao wa
twitter nchini Afrika Kusini unaonekana kupata umaarufu wakati nchi hiyo
inapokumbwa na viwango vikubwa vya ukosefu wa ajira.
Picha ya
mwanafunzi aliyefuzu chuo Anthea Malwandla imesambazwa kwa zaidi ya mara
1500 licha na picha hiyo kukosa kusababisha apate ajira.Anasema kuwa alifuzu kutoka chuo cha teknolojia cha Vaal na amekuwa akitafuta kazi kwa mwaka mmoja sasa.
Wiki iliyopita takwimu zilionyesha kuwa viwango vya ukosefu wa ajira ni asilimia 26.7, ikiwa ni asimia 12 zaidi mwaka huu.