Recent Posts

PropellerAds

Thursday, May 12, 2016

Orodha ya Mataifa fisadi zaidi Afrika Mashariki

Baada ya waziri mkuu wa Uingereza David Cameron
kunaswa na kamera akiidunisha Nigeria kuwa mafisadi
wakuu kote duniani BBC imeamua kuangazia kwa
umakini ikiwa matamshi hayo ni ya kweli.
Je Nigeria imeorodheshwa katika nafasi ipi katika
orodha ya mataifa fisadi kwa mujibu wa shirikisho la
kupambana dhidi ya ufisadi duniani Transparency
International ?
Ni vigumu kuelezea kwa kina ama hata kupiga msasa
ufisadi katika mataifa kwani kila mwanauchumi
anaelezea ufisadi akitumia mizani tofauti na mwenziye.
Kwa sababu hiyo tutatumia orodha ya mwaka wa 2015
ya shirikisho la kupambana dhidi ya ufisadi,
Transparency International, ili kukupa taswira ya
mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki na jinsi
yanavyolinganishwa na mataifa mengine duniani katika
mizani ya ubadhirifu na wizi wa mali ya uma.
Cha mno hata hivyo sharti tuweke bayana kuwa Nigeria
sio taifa fisadi zaidi duniani.
Nigeria imeorodheshwa katika nafasi ya 136 Nigeria
kati ya mataifa 167.
Kenya kwa mfano inasemekana kuwa na ufisadi
mkubwa hata kuishinda Nigeria.
Katika kanda ya Afrika Mashariki , mali ya umma
inafujwa sana na viongozi wa serikali hali ambayo
inaiweka mataifa ya kanda katika nafasi za mwisho
mwisho kuashiria viwango vya juu vya ufisadi.
Kati ya mataifa kumi Fisadi zaidi duniani Somalia
inaongoza ikifwatwa na Sudan ,Sudan Kusini, Eritrea,
Burundi, DRC, Uganda, Kenya Tanzania Ethiopia na
kisha Rwanda katika usanjari huo.
Somalia inaongoza kwa Ufisadi duniani katika nafasi ya
167.
Viwango vya ufisadi vinanasibishwa na Korea
Kaskazini.
Nchi iliyojitenga kabisa na ufisadi kanda ya Afrika
Mashariki na kati ni Rwanda.
Taifa hilo linaloongozwa na rais Paul Kagame
linaorodheshwa katika nafasi ya 44 duniani.
Je unakumbuka rais Robert Mugabe aliyewadunisha
wakenya kwa kuwa wezi ?
Kulingana na orodha hii iliyotayarishwa na shirika la TI
Zimbabwe wanaorodheshwa katika nafasi ya 150
duniani kwa ufisadi.
Wanagawana nafasi hiyo na Burundi.
Orodha ya mataifa 10 fisadi zaidi kanda ya Afrika
Mashariki na Duniani.
1. 167 Somalia / Korea Kaskazini
2. 165 Sudan
3. 163 South Sudan/ Angola
4. 154 Eritrea/Yemen / Turkmenistan / Syria
5. 150 Burundi / Zimbabwe
6. 147 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo / Chad /
Myanmar /
7. 139 Kenya / Uganda
8. 117 Tanzania
9. 103 Ethiopia
10. 44 Rwanda