Recent Posts

PropellerAds

Monday, May 9, 2016

Polisi watawanya wafuasi wa upinzani Nairobi

Cord
Polisi jijini Nairobi wametumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wa muungano wa upinzani Cord waliokuwa wameandamana hadi afisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC).
Waandamanaji hao, wakiongozwa na viongozi wa muungano huo, walitaka kuwashinikiza wakuu wa tume hiyo wajiuzulu.
Kiongozi wa Cord Raila Odinga, aliyekuwa wakati mmoja waziri mkuu, amesema viongozi hao hawawezi kusimamia uchaguzi huru na wa haki mwaka ujao.
Hii ni mara ya pili kwa muungano huo kufanya maandamano hadi afizi za IEBC.
Cord
Mwishoni mwa mwezi uliopita, polisi waliwatawanya tena kwa kutumia vitoa machozi.
Viongozi wa muungano huo wameapa kufika katika afisi za IEBC Jumatatu kila wiki hadi viongozi wa tume hiyo waondoke afisini

Related Posts:

  • Helmeti zatajwa kuwa chanzo cha maradhi ya ngoziDodoma. Wakati Sheria ya Usalama Barabarani inamtaka kila dereva wa bodaboda kuwa na kofia ngumu (helmeti) mbili kwa ajili yake na abiria, watumiaji wa vyombo hivyo wapo hatarini kuambukizwa maradhi ya ngozi. Hatari hiyo inat… Read More
  • Barafu kubwa kumeguka AntarcticaWanasayansi wameambia BBC kuwa barafu kubwa iliyo na ukubwa mara 50 kushinda kisiwa cha Manhattan, Marekani imefikia kiwango cha kupasuka kutoka eneo kubwa la barafu la Larsen C kaskazini mwa Antarctica. Siwa barafu hiyo inat… Read More
  • Laptop iliyo na screen tatu yazinduliwa Las VegasKampuni inayotayarisha michezo ya kompyuta ya Razer imezindua kipakatalishi (kompyuta ya kupakata/laptop) mpya ambayo ina screen tatu wenye maonyesho ya teknolojia mpya mjini Las Vegas. Kampuni hiyo imesema laptop hiyo ambayo… Read More
  • Tanzania haina njaa wala watu hawana njaa.Anaejua kuna njaa nchi hii ni Rais,mimi ndio naejua wapi kuna njaa na wapi hakuna.Tanzania hii haina njaa wala watu hawana njaa,anasema Rais JPM kutoka Simiyu Wanaotangaza kuna njaa ni watu wanaolipwa pesa na wafanyabiashara … Read More
  • Wasichana 800 wakeketwa kaskazini mwa TanzaniaWasichana zaidi ya 800 walikeketwa kaskazini mwa Tanzania mwezi uliopita, mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luoga amesema. Hilo lilifanyika ingawa polisi wamekuwa wakikabiliana na utamaduni huo. Wanawake 12 wanaotuhumiwa kuhu… Read More