Mama mmoja raia wa Australia ametoa picha za mapacha watano aliowazaa mwezi Januari.
Kim Tucci wa miaka 26 alichukua dadika mbili tu kujifungua wanawe hao, wasichana wanne na mvulana mmoja.
Wote walitungwa kawaida, hakutumia matibabu yeyote ya uzazi.
Madaktari 50 walimsaidia mama huyo kujifungua kwa njiya ya upasuaji,
na wanawe wote wako shwari.Wanasayansi wanasema ni mama mmoja kati ya
milioni 55 ana nafasi ya kuzaa mapacha watano.
Bi Tucci alipata
umaarufu sana wakati alipoweka taarifa za mimba yake katika ukurasa wake
wa Facebook.Kampuni ya kunasa picha ya Erin Elizabeth imesaidia sana
kunadi safari ya Bi Tucci wakati wa uja uzito wake.
Mama huyo ameelezea changamoto alizokumbana nazo akisema kwa wakati
mmoja alihisi kama anapoteza maisha.Ameongeza madaktari walimshauri
kuwaokoa watoto wawili na kumtaka kuwatoa wengine kutokana na sababu za
kiafya.
Hata hivyo aliamua kubeba mimba yake hadi mwisho.
Bi
Tucci na mumewe bwana Vaughn wana watoto watatu mvulana na wasichana
wawili.Wameanza kuchangisha pesa ili kununua gari kubwa ambalo litaweza
kukimu familia hiyo kubwa.
Anayedaiwa kumchoma moto mwanamke katika njia ya treni kufikishwa mahakamani
-
Mwanamume anayedaiwa kumchoma moto mwanamke aliyekuwa amelala hadi kufa
ndani ya treni ya chini ya ardhi ya Jiji la New York anatarajiwa kufikishwa
mahak...
15 hours ago