Picha ya mwanamuziki Justin Bieber
akimpiga busu aliyekuwa mpenziwe Selena Gomez ndio picha iliopendwa na
wengi katika mtandao wa instagram.
Imependwa na watu milioni 3,569,000 huku watu 350,000 wakiipenda dakika 15 tu baada ya kuchapishwa.Picha hiyo iliokuwa na maelezo chini yake yalioandikwa ''Feels'' imeipiku picha ya Kendal Jenner ambayo ndio picha iliopendwa sana.
Pia nayo imezungumziwa karibu mara milioni.
Selena na Justin waliachana mwaka 2014 lakini mtandao haujamalizana na ''Jelena''.
Pia Bi Gomez aliipenda baada ya Justin Bieber kuichapisha.Justin Bieber sasa ana takriban wafuasi milioni 70 katika mtandao wa Instagram.