Rais wa Marekani Barack Obama
amewahimiza wanafunzi 2,000, wengi wao weusi kuimarisha juhudi za
kupambana na ubaguzi wa rangi aliosema umebakia nchini humo.
Akizungumza
katika Chuo Kikuu cha Howard mjini Washington, Bw Obama alisema hali
ya Wamarekani wenye asili ya Kiafrika imeimarika sana tangu yeye atoke
chuo kikuu mwaka 1983.
Lakini alisema kuchaguliwa kwake kwa rais wa kwanza mwenye asili ya Afrika nchini humo hakujasaidia kupunguza ubaguzi wa rangi.
Bwana Obama alisema vijana hao wanapaswa kujivunia kuwa watu weusi lakini lazima wahakikishe kuwa wana mipango kambambe ya kuleta mabadiliko.
Bwana Obama alisema vijana hao wanapaswa kujivunia kuwa watu weusi lakini lazima wahakikishe kuwa wana mipango kambambe ya kuleta mabadiliko.