Profesa wa uchumi kutoka Italia, ameelezea hasira za
kucheleweshwa katika angatua ya Philadelphia
Marekani kwa sababu eti mmoja wa abiria aliyekuwa
ameketi karibu yake alimshuku kuwa gaidi kwa sababu
alikuwa akifanya hisabati.
Profesa Guido Menzio anasema kuwa alicheleweshwa
kuabiri ndege aliyokuwa amepanga kusafiri nayo
akihojiwa na maafisa wa usalama wa uwanja huo wa
ndege.
Yamkini mwanamke mmoja alikuwa amewanong'onezea
maafisa hao kuwepo kwa tishio la usalama kutokana na
hisabati ya Profesa huyo.
Profesa Menzio, mwenye nywele nyeusi na rangi ya
hudhurungi alikuwa ameratibiwa kupanda ndege
iliyokuwa ikitokea Philadelphia, Marekani.
Mwanamke huyo kwa mujibu wa Profesa Menzio
alionekana kuwa na hofu.
Kisirisiri mwanamke huyo alipitisha ujumbe kwa
mhudumu mmoja wa ndani ya ndege alipomuona
profesa akifanya hesabu, alimfikiria kuwa ni gaidi..
Professor Menzio tena alihojiwa kwa urefu na rubani na
afisa mmoja.
Baadaye alisema, itifaki ya usalama ya shirika hilo la
ndege ni ngumu sana , na inategemea abiria ambao
pengine ni wajinga.
Anayedaiwa kumchoma moto mwanamke katika njia ya treni kufikishwa mahakamani
-
Mwanamume anayedaiwa kumchoma moto mwanamke aliyekuwa amelala hadi kufa
ndani ya treni ya chini ya ardhi ya Jiji la New York anatarajiwa kufikishwa
mahak...
15 hours ago