Mawakili wa Moise Katumbi wanasema Gavana huyo wa zamani wa jimbo lililo na utajiri wa madini - Katanga, alikabidhiwa barua ya kufika mahakamani mwishoni mwa juma na anatakiwa kufika mbele ya mwendesha mashtaka nchini humo siku ya Jumatatu.
Nyumba yake ilisakwa na walinzi wa serikali siku ya Jumamosi.
Katumbi amekana mashtaka na ameishutumu serikali kwa kutumia njia za kumchafulia jina.
Ubalozi wa Marekani mjini Kinshasa pia umetilia shaka tuhuma hizo.
Rais Joseph Kabila ambaye yupo madarakani tangu mwaka 2001 bado hajabainisha iwapo atajiuzulu mwaka huu kama inavyo takiwa kwenye katiba ya nchi