Taifa la Zimbabwe linatarajiwa kuchapisha dola zake kama zile za Marekani ili kukabiliana na upungufu wa fedha nchini humo.
Gavana
wa benki kuu nchini humo John Mangudya amesema kuwa fedha hizo
zinazojulikana kama fedha za dhamana zitafadhiliwa na dola milioni 200
kutoka kwa benki ya kuagiza na kuuza nje ya Afrika.Noti hizo za dola 2,5, 10 na 20 zitakuwa na thamani sawa na dola ya Marekani.
Zimbabwe ilizindua dola ya Marekani baada kuiwacha sarufi yake mwaka 2009 kufuatia kupanda kwa mfumuko.
Tangu wakati huo raia wa Zimbabwe wamekuwa wakitumia dola pamoja na sarufi nyengine za kigeni ikiwemo randi ya Afrika Kusini na Yuan ya China.
Lakini gavana wa benki kuu amesisitiza kuwa hiyo sio hatua ya kwanza ya kurejesha utumizi wa sarufi ya Zimbabwe kulingana na gazeti la The Herald.
Bw Mangudya pia alianzisha hatua kadhaa za kuwazuia watu kutumia dola ya Marekani.
Anataka kuwapa moyo watu kutumia sarufi ya randi kwa sababu idadi kubwa ya biashara ya Zimbabwe inafanyika kati ya taifa hilo na Afrika Kusini.