Recent Posts

PropellerAds

Thursday, May 12, 2016

Trump alegeza msimamo kuhusu Waislamu

Mgombea Urais wa Republican anaonekana kulegeza
msimamo kuhusiana na pendekezo lake tata la
kuwazuia Waislamu kuingia Marekani.
Katika mahojiano na kituo cha television cha Fox News,
Donald Trump akijibu kauli ya meya mpya wa mji wa
London Sadiq Khan, ambaye awali alionyesha wasiwasi
na kusema hataweza kuingia nchini Marekani chini ya
utawala wa Donald Trump, Trump ameiambia Fox News
kwamba meya huyo anaweza kuja kwani hayo yalikuwa
ni maoni tu.
Hata hivyo, Bwana Khan amekataa ukarimu huo wa
Trump ambao unamlenga yeye pekee na sio kwa ajili
ya jamii yote ya waislamu.
Pendekezo la kuwazuia waislamu kuingia nchini
Marekani lilipata upinzani mkubwa ndani na nje ya
Marekani.
US: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama
Trump akemewa kwa matamshi kuhusu Waislamu
Wakati huo huo, Waziri mkuu wa Uingereza, David
Cameron, ameomba msamaha kwa kiongozi wa dini ya
kiislamu baada ya kumtaja kuwa ni mfuasi wa kundi la
Islamic State.
Cameron alitoa kauli hiyo bungeni wiki tatu zilizopita
katika kampeni za kutafuta meya mpya wa London.
Bwana Cameron amesema mgombea wa upinzani Sadiq
Khan - ni muislamu aliyeshinda kiti hicho cha umeya,
ameonekana mara kadhaa na iman Sulaiman Ghani,
imamu mstaafu.
Kwa upande wake, Iman Ghani ametishia kuchukua
hatua za kisheria kutokana na madai hayo kwamba
yeye ni mfuasi wa Islamic State.

Related Posts:

  • Will We Be Finally ‘Saved’ by Faith Alone? The biblical term salvation is used to cover past, present, and future dimensions of God’s work to bring us into everlasting perfection and joy. Ephesians 2:8 says, “You have been saved.” … Read More
  • I Will Not Lie with You The battle against sexual temptation isn’t won simply with Internet filters and accountability partners. It is won with Spirit-filled convictions, which over time produce new affections and desires. Filters and friends are… Read More
  • 10 Things to Know about Speaking in Tongues The spiritual gift of speaking in tongues remains controversial in our day and is a subject deserving of our close attention. This short article is not designed to argue that tongues are still valid but simply attempts to d… Read More
  • Every Small Group Needs a Vision Your small group is destined to die a slow, complacent, even cordial death without direction. Good food and casual conversation might be staples of normal small group life, but they cannot be the substance. Too many groups… Read More
  • Joy Drives Us “Therefore God has highly exalted him and bestowed on him the name that is above every name, so that at the name of Jesus every knee should bow, in heaven and on earth and under the earth, and every tongue confess that Jes… Read More