Recent Posts

PropellerAds

Friday, May 6, 2016

Mfanyabiashara Jacob Juma auawa Nairobi


Juma

Mfanyabiashara mashuhuri Jacob Juma, ambaye amekuwa akizua mjadala mitandaoni Kenya kutokana na ujumbe wake anaoandika hasa kwenye Twitter, ameuawa kwa kupigwa risasi jijini Nairobi.
Taarifa zinasema Bw Juma alipigwa risasi na watu ambao walikuwa wakiendesha pikipiki alipokuwa akielekea nyumbani kwake mtaa wa Karen mwendo wa saa nne usiku.
Gari lake lilipatikana na zaidi ya matundu 10 ya risasi.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya, polisi wanasema hakuna kilichoibiwa kutoka kwenye gari lake. Simu zake mbili na pesa vilipatikana ndani ya gari.
Bw Juma alikuwa mwanakandarasi ambaye pia alihusika katika sekta ya uchimbaji madini.

 
Alikuwa mkurugenzi katika kampuni ya Erad iliyoshtaki Bodi ya Taifa la Nafaka na Mazao kuhusu kandarasi. Alitaka alipwe jumla ya Sh500m na bodi hiyo.
Agosti mwaka jana, alimshtaki Gavana wa jiji la Nairobi Dkt Evans Kidero akitaka akaunti zake za benki zifungiwe kwa tuhuma kwamba gavana huyo alihusika katika ufujaji pesa kampuni ya sukari ya Mumias Sugar.
Bw Juma pia alimshtaki waziri wa madini Najib Balala mwaka jana baada ya leseni ya kampuni yake ya madini ya Cortec Mining kupokonywa leseni.
Miaka 10 iliyopita, kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, Bw Juma pia alimshtaki bintiye rais wa zamani Daniel arap Moi kuhusiana na shamba la ekari 250.
Aidha, aliwasilisha kesi mbili dhidi ya Naibu Rais William Ruto.
Amekuwa akikosoa sana serikali ya Rais Uhuru Kenyatta na ni mmoja wa waliokuwa wakiishinikiza sana kuhusiana na sakata ya Eurobond.

Related Posts:

  • Mkewe Obama amtambua mbunifu kutoka KenyaMkewe rais wa Marekani Michelle Obama amemsifu mjasiria mali kutoka Kenya mwanzilishi wa kampuni inayotengeza biadhaa za watoto bi Wanjiru Waithaka Waweru. Katika dhifa ya jioni iliyoandaliwa kwa heshma ya wanawake bi Wanjir… Read More
  • TZ yataka uzoefu wa Qatar sekta ya gesiRais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa taifa lake linakusudia kufanya biashara na jamhuri ya Qatar haswa katika sekta ya gesi na usafiri wa ndege. Rais Magufuli aliyasema hayo baada ya kukutana na balozi wa Q… Read More
  • Miaka 90 jela kwa kunajisi wanafunziMwalimu mmoja wa shule ya msingi katika eneo la kati nchini Kenya amehukumiwa kifungo cha miaka 90 jela kwa kuwanajisi wanafunzi wake. Hii ni moja kati ya vifungo vya muda mrefu zaidi kuwahi kutolewa kwa watu wanaodhulumu wa… Read More
  • Philadelphia na kodi ya vinywaji Katika mji wa Philadelphia nchini Marekani wameanza kutoza kodi ya vinywaji vyenye sukari na kaboni licha ya kuwepo kwa mamilioni ya kampeni zilizofanywa na kampuni za vinywaji baridi kutaka kufungwa. Meya wa demokrasia ya … Read More
  • Auawa akichuma kuvu yenye 'nguvu za kiume'Mtu mmoja amepigwa risasi na kuuawa katika kijiji cha Nepal alipokuwa akichuma kuvu fulani inayotambuliwa kwa uwezo wake wa kuongeza nguvu za kiume. Kuvu hiyo inayotambulika kama ''Himalayan Viagra'' inasemekana kuwaongezea … Read More