Nchi ya Nigeria imekumbwa na uhaba mkubwa wa
nyanya. Asilimia themanini ya mashamba ya nyanya
katika maeneo ya kaskazini inasemekana
yameharibiwa na watoto wanaokula kila kitu.Matokeo
yake, bei ya bidhaa hiyo imepanda maradufu.
Mji wa Kura, ni mji ambao unajulikana kwa kilimo cha
umwagiliaji kilomita thelathini magharibi mwa mji wa
Kano uliopo kaskazini mwa Nigeria.
Badala ya majani ya kijani na matunda yake yenye
rangi nyekundu, ninachokiona hapa ni majani madogo
yaliyokauka. Hii ni ishara tosha kwamba Tuta absoluta,
mdodo ambae anakula mizizi, mti, majani na matunda
yuko hapa. Mashamba mingi hapa yana muonekano
sawa. Shamba la Dahiru Dantsoho ni miongoni mwa
yaliyoathirika:
Kura "hii imesababishwa na mdudu tunaemuita sharon
ambae anakula mti ikiwemo mizizi, na huacha shamba
likiwa limeungua. Tumetumia dawa mbalimbali lakini
hazikusaidia, hii imepangwa na Mungu."
Wakulima wanaangalia kwa kukata tamaa jinsi tunda
walilolifanyia kazi, likiangamia. Muhammad Idris Kura ni
mmoja wa wakulima ambae anasema hata hawezi
kuanza kuhesabu hasara walioipata:
Muhammad Idris Kura: anasema "kwa kweli siwezi
kukisia hasara niliyoipata, kwa sababu tumefanya
baadhi ya kazi hapa sisi wenyewe. Iwapo tutakadiria
gharama ya jasho letu, kiwango kitakuwa kikubwa mno,
ni kwa sababu hiyo ndio maana hatuhesabu. Kwa
mfano hivi sasa, hawa wakulima hawana mbolea ya
kutumia mashambani mwao hasa katika msimu wa
mvua na hawana chakula pia. Hakuna kitu
wanachoweza kufanya zaidi ya kukubali matokeo. "
katika jimbo jirani la Kaduna, serikali imekisia kwamba
takriban asilimia themanini ya mashamba ya nyanya
yameharibiwa, huku wakulima mia mbili katika jamii
tatu wakipata hasara ya zaidi ya dola za kimarekani
laki tano.Hata hivyo, serikali ya Nigeria imesema
imewapa kazi wataalamu kuliangalia tatizo hilol ambalo
limeathiri majimbo sita.
Katika mji wa Kano, hasara hiyo imekilazimu kiwanda
cha nyanya ambacho kimeanzishwa na mfanyabiashara
maarufu, Aliko Dangote, kufungwa kutokana na uhaba
wa bidhaa hiyo.
Anayedaiwa kumchoma moto mwanamke katika njia ya treni kufikishwa mahakamani
-
Mwanamume anayedaiwa kumchoma moto mwanamke aliyekuwa amelala hadi kufa
ndani ya treni ya chini ya ardhi ya Jiji la New York anatarajiwa kufikishwa
mahak...
16 hours ago