Recent Posts

PropellerAds

Friday, May 13, 2016

UN: Rwanda bado inasaidia waasi Burundi

Rwanda
Ripoti ya siri iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa inaituhumu Rwanda kwa kuendelea kuwasaidia waasi wanaotaka kumtoa madarakani Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Rwanda imekuwa ikitoa mafunzo, ufadhili na usaidizi wa kimipango kwa waasi hao.
Baadhi ya maafisa wan chi za Magharibi wamekuwa wakidhani hilo lilikoma baada ya kutolewa kwa ripoti nyingine mwaka jana, lakini ripoti hiyo inasema hali ni kinyume.
Kamati ya Baraza la Usalama la UN inayoshughulika na vikwazo itajadili ripoti hiyo baadaye leo Ijumaa.
Rwanda amekana madai hayo kwamba inaingilia katika masuala ya ndani nchini Burundi.
Rais Nkurunziza alichaguliwa kwa muhula wa tatu mwezi Julai mwaka jana.
Nkurunziza
Machafuko yalizuka nchini humo baada yake kutangaza angewania kwa muhula mwingine mwezi Aprili mwaka jana.
Jaribio la mapinduzi lilitekelezwa mwezi Mei lakini halikufanikiwa.