Recent Posts

PropellerAds

Thursday, May 12, 2016

Besigye akamatwa kwa 'kujiapisha' Uganda

Taharuki imetanda nchini Uganda baada ya kiongozi
wa upinzani Dr Kizza Besigye, ''kujiapishwa kama rais''
siku moja tu kabla ya kuapishwa rasmi kwa rais
Yoweri Museveni .
Haijulikani ni vipi Dr Kiiza Besigye alikwepa kizuizi cha
polisi na kuibukia mjini Kampala ambapo alikutana na
wandani wa chama chake na ''kula kiapo cha urais wa
taifa hilo''.
Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii
Dr Besigye anaonekana ''akila kiapo'' mbele ya mtu
aliyevalia mavazi sawa na ya ''jaji wa mahakama ya
juu''.
Video hiyo imesambazwa mno kwenye mitandao ya
kijamii na kusababisha mamlaka inayosimamia
mawasiliano nchini Uganda kuamrisha kampuni
zinazotoa huduma za simu nchini humo kufunga
huduma za mitandao ya kijamii.
Besigye anahitimisha 'kuapishwa kwake'' kwa kuonya
kuwa ''endapo kutafanyika sherehe nyengine hapo
kesho, basi itakuwa ni kinyume cha sheria kwani
kulingana naye Museveni hakushinda uchaguzi
wowote''.
Mgombea huyo wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama
cha upinzani cha Forum for democratic change FDC-
alikamatwa na polisi kwa'' kukaidi amri halali''.
Matukio hayo yanawadia wakati ambao viongozi wa
kanda ya Afrika Mashariki na wageni mashuhuri
wameanza kuwasili mjini Kampala ilikuhudhuria
kuapishwa kwa rais Museveni hapo kesho.
Tangu matokeo ya uchaguzi kutangazwa mwezi
Februari, Dr Kiiza Besigye amekuwa chini ya ulinzi
mkali nyumbani kwake baada ya kupinga matokeo
yaliyompa rais Museveni ushindi.