Recent Posts

PropellerAds

Sunday, May 8, 2016

Mwana harakati apigwa risasi pakstani

Mwandishi wa habari ambaye pia ni mkereketwa wa
haki za kibinadamu, Khurram Zaki, amepigwa risasi na
kuuawa jijini Karachi, Pakistan.
Ripoti zinasema kuwa alikuwa akila chakula katika
mgahawa mmoja wakati alipopigwa risasi na washukiwa
wanne waliokuwa kwenye pikipiki.
Watu wengine wawili walijeruhiwa vibaya katika
shambulio hilo.
Khuram Zaki alikuwa mhariri wa gazeti moja kwenye
mtandao lijulikanalo kama "Tujenga Pakistan , ambalo
linashutumu mgawanyiko na kuitisha ustawi wa
demokrasia na maswala yasiyoandamana na dini.
Ukereketwa wake wa hivi majuzi ni kuwashutumu wale
waliochochea chuki na uhasama dhidi ya Waislamu
Washia.
Majuzi tu alikashifu udhalilishwaji wa imamu wa msikiti
mwekundu ulioko Islamabad.
Bw Zaki na wengine walikwenda mahakamani
kumshtaki bwana Abdul Aziz kwa kuchochea uhasama
dhidi ya waislamu wachache wa kishia.
Madai hayo yanatokana na kauli ya kadhi huyo kukataa
katakata kukashifu shambulizi la kigaidi katika shule
moja mjini Peshawar mwaka wa 2014 ambapo
wanafunzi 152 waliuawa.