Recent Posts

PropellerAds

Wednesday, May 18, 2016

Besigye ashtakiwa kosa la uhaini Uganda

BesigyeKiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye amefikishwa mahakamani mjini Kampala na kushtakiwa kwa kosa la uhaini.
Dkt Besigye alifikishwa katika majengo ya mahakama ya Nakawa mapema kabla ya saa tatu, muda wa kawaida wa kufunguliwa kwa mahakama, na akasomewa mashtaka
.
Alijiwakilisha mwenyewe kortini na amesema hataki kuhusisha mawakili katika kesi hiyo.
Hakimu ameamuru awekwe rumande hadi tarehe 1 Juni.
Dkt Besigye ndiye aliyekuwa mpinzani mkuu wa Rais Yoweri Museveni kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Februari nchini humo.
Leo imekuwa mara ya pili kufikishwa mahakamani akikabiliwa na tuhuma hizo za uhaini kwani awali alifikishwa mahakani kwa mara ya kwanza siku ya Ijumaa iliyopita katika mji wa Moroto, baada yake kudaiwa kujiapisha kuwa rais siku moja kabla ya Rais Museveni, aliyetangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo kuapishwa..
Besigye alishikiliwa na polisi kwa muda wa siku mbili ambapo alifikishwa mahakamani huku shughuli za mahakama zikiwa zimekwisha.
Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wafuasi wake ambao wamekuwa wakisema hakuruhusiwa kuwasiliana na wanasheria wake