Recent Posts

PropellerAds

Monday, May 2, 2016

Mjue Ndovu

https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/d/dc/Elephant_near_ndutu.jpg
Ndovu au tembo ni aina za wanyama wenye umbo kubwa kupita wanyamapori wote. Watoto wake wakizaliwa hufikia kg 100 na ndovu mzima huwa na uzito wa tani 2 hadi 5; kimo ni hadi m 4.
Kibiolojia ni mamalia. Sehemu ya pekee mwilini ni mwiro ambao hali halisi ni pua la tembo lililorefuka na kufanya kazi pia kama mkono wake yaani kwa kutumia mwiro ndovu hushika vitu na kufanya utafiti kwa kugusagusa.

Pembe-jino zake zinatafutwa sana kama mapambo na biashara ya pembe za ndovu imeshakuwa hatari kabisa kwa ndovu wote kwa sababu wanawindwa mno. Hivyo kwa mapatano ya kimataifa biahsara ya pembe hizi imepigwa marufuku.
Image result for jino la tembo picture

Spishi

Kwa jumla kuna spishi tatu za ndovu ambao wanafanana lakini hawazai pamoja. Ndovu-nyika ni mkubwa kuliko wengine.
Ndovu wa Asia ni mdogo wake lakini anazoea wanadamu kwa hiyo katika nchi kama Uhindi au Uthai hutumiwa kama mnyama wa kazi akibeba mizigo au watu. Zamani spishi hii ilitumiwa hata vitani. Kwa mfano jemadari Hanibal wa Karthago alishambulia Dola la Roma kwa msaada wa ndovu wa kijeshi waliovuka milima ya Alpi.
Ndovu-misitu alitazamiwa muda mrefu kama nususpishi ya Ndovu wa Afrika lakini wataalamu wamethebitisha ni spishi tofauti. Hufikia kimo cha mita 2 tu anaishi hasa katika misitu ya Kongo.


Chakula

Ndovu hula manyasi na majani mengi. Kwa chakula hiki ambacho ni kigumu hutegemea meno yao. Meno haya pole yanachakaa kutokana na ugumu wa manyasi na baada ya kuharibu meno yote ndovu hufa.
Penye ndovu wengi mno wanaharibu miti. Wanapenda majani ya miti na hivyo wanavunja matawi ili wapate majani. Wakiweza wanaangusha pia mti wote kwa chakula hiki. Uharibifu huu ni tatizo katika mbuga za wanyama kadhaa ambako ndovu haziwzi kutoka nje kwa sababu nje wanavindwa.


Tembo wa Africa


Ndovu-nyika - Mikumi.
Tembo wa Jenasi ya ‘Loxodonta’, kwa ujumla hujulikana kama tembo wa Africa. Kwa sasa wanapatikana katika nchi 37. Tembo wa Africa hutofautishwa na tembo wa Asia kwa namna mbali mbali. Kwanza masikio yao ni makubwa sana na mwili wao ni mkubwa wenye mgongo uliopinda. Wote, dume na jike wa tembo wa Africa huwa na pembe za ndovu/vipusa kwa nje na miili yao huwa na nywele kidogo kuliko tembo wa Asia. Ndovu wa Africa hugawanywa kwenye makundi mawili kulingana na spishi zao, ndovu-nyika (Loxodonta africana africana) na ndovu-misitu (Loxodonta cyclotis). Tembo wa savanna wa Africa, ndiyo tembo mkubwa kuliko wote. Ndiyo mnyama wa ardhini aliye mkubwa kuliko wote, huku tembo dume akiwa na urefu wa mita 3.2 mpaka 4 mabegani na uzito wa kg. 3,500 mpaka 12,000. Tembo jike huwa mdogo kiasi huku wengi wakiishia urefu wa mita 3 tu.
Wengi wa tembo wa savanna wa Africa hupatikana katika nyika, mabwawani, na kwenye fukwe za ziwa. Hukaa sana kwenye kanda za savanna kusini mwa jangwa la Sahara. Spishi nyingine ya ndovu wa Africa ni ndovu-misitu (Loxodonta cyclotis), ambao ni wadogo na wa mviringo kiasi, pembe zao zikiwa fupi kiasi na zilizonyooka kuliko tembo wa savanna. Tembo wa misituni hufikia mpaka uzito wa kg. 4500 na husikia urefu wa mita 3. Mambo mengi hayafahamiki kuhusu tembo hawa ukivilinganisha na tembo wa savanna, kutokana na mazingira wanamoishi. Mara nyingi huishi katika misitu ya Africa, ile mizito nay a mvua, ya kati na magharibi mwa Africa. Japo mara chache husogea mipakanai mwa misitu yao, na kuzaliana na tembo wa savanna.

Pembe

Image result for jino la tembo picture

Pembe za tembo wa Africa na Asia; Pembe za tembo ni kama meno ya pili ya chonge ya tembo hawa. Pembe hukua mfululizo, na kwa mwaka mmoja, huongezeka kwa sm 18 kwa tembo dume. Pembe hizi hutumika kuchimba kwa ajili ya maji, chumvi, miziz, kula magome ya miti, na kutaboa miti ya mibuyu kupata majimaji ya ndani. Pia hutumika kusafisha njia kwa kusogeza na kukata miti na matawi ya miti mikubwa. Pia hutumika kuweka alama kwenye miti kuonyesha mipaka ya hiamaya zao na mara kadhaa hutumika kama silaha.
Image result for jino la tembo picture
Kama ilivyo kwa binadamu, wanapokuwa wanazoea kutumia sana mkono wa kulia ama kwa wengine wa kushoto, vivyo hivyo tembo nao huwa na ubobezi katika kutumia aidha pembe ya kushoto au kulia. Pembe inayotumika sana, huitwa penge kuu, kuwa fupi kidogo, na iliyolika kidogo kwenye ncha yake kutokana na matumizi. Tembo wote wa Africa, dume na jike huwa na pembe kubwa zinazoweza kufikia mita 3 kwa urefu na uzito wa kilo tisini. Tembo wa Asia huwa na pembe kwa dume pekee, lakini pembe zao huwa nyembamba na nyepesi, huku nzito kuliko zote kwao ilikuwa na uzito wa kg 39 Pembe kwa spishi zote huundwa kwa kalsiamu fosfeti, huku sehemu ya tishu hai ikiwa ni ndogo mno. Watu hutaka kupata pembe za tembo kwa wingi nao kumepelekea sana kuadimika kwa tembo hao kutokana na uwindaji wa tembo.

Ngozi

Tembo wana ngozi pana sana kwenye asilimia kubwa ya msuli wao na hukaribia sentimeta 2.5 kwa upana. Japo ngozi kwenye mdogo na sikioni ina upana wa karatasi tu. Ngozi ya tembo wa Asia huwa na nywele kiasi, hasa wakati wa utoto na kupungua wakati wanapoendelea kukua; huku tembo wa Africa wakiwa hawana nywele kabisa.