Monday, May 2, 2016
Home »
» CIA yasema al-Qaeda wamedhoofishwa sana
CIA yasema al-Qaeda wamedhoofishwa sana
By The Cafe 4:02:00 AM
Mkurugenzi mkuu wa shirika la ujasusi la marekani CIA John Brennan anasema kwa Marekani imeangamiza sehemu kubwa ya mtandao wa Al Qaeda miaka mitano tangu kiongozi wake Osama Bin Laden auawe na vikosi maalum nchini Pakistan.
Bw Brennan alisema kuwa Bin Laden alikuwa mwenye ushawishi mkubwa na ilikuwa muhimu kumuondoa mtu ambaye alihusika na kupanga na mashambulizi ya Sepetemba 11 katika miji ya New York na Washington. Mkuu huyo wa CIA pia anasema kuwa ikuwa mkuu wa kundi la Islamic State, Abu Bakr Al-Baghdadi, atauawa itakuwa na athari kubwa kwa kundi hilo.