Meli ya kifahari ya Marekani imeanza
safari yake kuelekea Cuba ikitokea nchini Marekani kwa mara ya kwanza
katika kipindi cha zaidi ya miaka hamsini iliyopita.
Meli hiyo
iitwayo Adonia, imebeba abiria wapatao mia saba,imeng'oa nanga kutoka
katika bandari ya Miami na inatarajiwa kufika tamati ya safari yake
Jumatatu ijayo.Cuba na Marekani zimerejesha uhusiano baina yao wa kidplomasia mwaka wa jana, ingawaje vita baridi iliyokuwa baina ya nchi hizo ilisababisha hali kibiashara kati yao kuwa ya kusua sua na bado hali si shwari mpaka sasa.