Maelfu ya waombolezaji walijitokeza
kuadhimisha misa ya wafu kwa heshima ya mwanamuziki nyota wa muziki wa
Soukus na Rhumba raia wa Jamhuri ya Congo Papa Wemba.
Waomboloezaji
walipiga foleni ilikupata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho kwa
msanii huyo nguli aliyeaga dunia juma lililopita alipokuwa akiwatumbuiza
mashabiki wake huko Abidjan Ivory Coast.Mwili wake umewekwa katika majengo ya bunge mjini Kinshasa.
Serikali imetangaza siku tatu za maombolezi kuanzia leo hadi jumatano atakapozikwa.
- Maelfu watarajiwa kujitokeza kumuaga Papa Wemba
- Faly Ipupa na mashabiki waulaki mwili wa Papa Wemba
- Historia ya Papa Wemba
Wengi waliitambua sauti hiyo ya na utunzi wake.
Alikuwa ni mtumbuizaji kamili.
Gwiji huyo wa muziki wa Lingala alizaliwa mnamo Juni 14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu - Wilaya ya Sankuru nchini Congo.
Jina lake halisi ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba.
Yeye alianza kazi ya muziki akiwa na umri mdogo mno.
Alikuwa akimfuata mamake katika matanga na hivyo akaibukia kuwa mtunzi wa nyimbo za kuomboleza.
Mfalme huyo wa muziki wa Rhumba, mwenye umri wa miaka 66 aliaga dunia ghafla 24 April akiwa nchini Ivory Coast .