Maafisa wanne wa polisi nchini China
watashirikiana na wenzao wa Itali kupiga doria mjini Rome na Milan
katika jaribio la wiki mbili.
Maafisa hao wanaozungumza Kitaliano
wanatumwa nchini Itali kwa lengo la kuwafanya watalii wa China kujisikia
huru na salama wakati huu wa msimu wa juu wa utalii,amesema waziri wa
maswala ya ndani nchini humo Angelino Alfano.''Iwapo jaribio hilo litafanikiwa,tutafanya hivyo kwa miji mingine nchini Italy'',alisema.
Takriban watalii milioni 3 wa China hutembelea Itali kila mwaka.
Bwana Alfano alisema kuwa maafisa wa Itali hivi karibuni wataanza kuelekea Beijing na Shanghai kupiga doria wakishirikiana na maafisa wa China.