Tume ya haki za kibinaadamu nchini
Afrika Kusini imetakiwa kuchunguza tamko la ubaguzi wa rangi
lililochapishwa na Matthew Theunissen ambalo limezua hisia kali katika
mitandao ya kijamii.
Hatua hiyo inajiri baada ya tamko la bw
Theunissen kuhusu hatua ya waziri wa michezo Fikile Mbalula kupiga
marufuku mashiriksho ya michezo kuwania kushiriki katika michuano ya
kimataifa kutokana na idadi ndogo ya wachezaji weusi katika timu.Raga,Kriketi na riadha zimeathiriwa.
Bw Theunissen:Kwa hivyo hakuna michezo Afrika Kusini.
Baadaye alitumia matamshi ya kibaguzi na matusi kuikosoa serikali.
Chapisho hilo limevutia shutuma kali kutoka kwa raia weusi na wazungu nchini Afrika Kusini.
Taifa hilo kwa sasa linaangalia ubaguzi wa rangi kama adhabu kubwa.