Watu maarufu katika tamasha la sanaa ya makavazi mjini New York
walivalia mavazi ya vyuma huku wakisheherekea mkutano wa binaadamu na
Mashini.
Hatahivyo sio wote waliohudhuria tamasha hilo walivaa kulingana na madhari ya tamasha hilo.
Tamasha hilo la kila mwaka huiletea mamilioni ya fedha taasisi ya nguo za makavazi.
Mwaka uliopita wale waliohudhuria tamasha hilo walitakiwa kuvaa
kulingana na mandhari ya ushawishi wa China katika fesheni za
kimagharibi na kulikuwa na ufanisi mkubwa
Tiketi mwaka huu ziliuzwa kwa dola 30,000 kwa mtu mmoja,lakini licha ya
bei hizo za tiketi ni sherehe ambayo ni vigumu kuhudhuria.
Faragha ya wageni hulindwa sana,na uchapishaji wa mitandao ya kijamii
baada ya kuingia katika zulia jekundu umepigwa marufuku tangu mwaka
jana.
Mwaka uliopita zaidi ya dola milioni 12 zilichangishwa katika taasisi hiyo ya mavazi ya makavazi.
Majeneza yapangwa katika mitaa ya Jerusalem kwa maandamano
-
Waandamanaji wa mrengo wa kulia walianza kuandamana Jumatano usiku kupinga
makubaliano ya kusitisha vita vya Gaza ambayo yatashuhudia kuachiliwa kwa
anga...
1 hour ago