Kaunti ya California imethibitisha kifo chake kupitia ujumbe wa Twitter.Hakuna maelezo zaidi yaliotolewa.
Alice Faye Williams,alibadilisha jina lake na kuitwa Shakur akiwa mtu mzima alipokuwa mwanaharakati wa kisiasa na kujiunga na vuguvugu la Black Panther.
Alikuwa na mimba ya Tupac mwaka 1971 alipokamatwa na kufungwa jela pamoja na wanachama wengine wa vuguvugu hilo na kukabiliwa na mashtaka ya njama ambayo baadaye yalitupiliwa mbali.
Shakur alikuwa kigezo kizuri cha muziki wa mwanawe na alisimamia mziki wake baada ya kifo chake.
Mauaji yake bado hayajapata ufafanuzi.