Polisi India wamesema kuwa kijana mmoja amejipiga
risasi kichwani kimakosa,akitafuta mbinu ya kujipiga
picha ya ''selfie'' ya kipekee akiwa na bastola ya
babake.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 15 anaendelea
kupokea matibabu katika hospitali kuu ya Pathankot
iliyoko katika jimbo la Punjab
Yamkini ajali hiyo ilitokea ijumaa jioni kijana huyo
aliporejea nyumbani akitoka shuleni .
Walioshuhudia wanasema kuwa alichukua bastola ya
babake iliyoidhinishwa na serikali lakini kwa bahati
mbaya akajipiga risasi kichwani akitaka kupiga selfie
akiwa ameshika bastola kichwani.
Tukio hilo limevutia hisia kali miongoni mwa wenyeji
ambao bado wanaomboleza kifo cha kijana mwengine
aliyekanyagwa na treni akijaribu kupiga selfie kwenye
reli huku gari moshi likija kwa kasi.
Takriban nusu ya idadi ya vifo vya watu 27 vilivyotokea
kote duniani mwaka wa 2015 kutokana na picha za
''selfie'' vimetokea nchini India.
Bashungwa awakutanisha polisi na LATRA kujadili mikakati ya kuzuia ajali za
barabarani
-
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ameongoza kikao
kilichoikutanisha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jeshi la Polisi
Tanzania pamoja ...
1 hour ago