Msanii Snura Mushi ambaye wimbo wake
wa Chura ulipigwa marufuku na serikali ya Tanzania ameomba radhi na
kuahidi kutekeleza maagizo ya serikali.
Wimbo huo ulipigwa
marufuku na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo ilisema
"maudhui ya utengenezwaji wa video ya wimbo huo “haiendani na maadili ya
Mtanzania.”Mamlaka hiyo ilisema kazi hiyo inadhalilisha tasnia ya muziki.